Kutoka Amsterdam hadi duniani kote

Tunawekeza kwenye kazi zako

Sonomo inanunua haki za muziki, kisha inaufanya muziki huo usikike zaidi.

Pata tathmini yakoInachukua dakika 3–5
Jinsi ya kuuza katalogi yako

Hatua tatu hadi pesa iingie kwenye akaunti yako.

01Tuma katalogi yako
Tuma katalogi yako
Dakika chache za kujibu maswali kuhusu muziki wako, nani anamiliki haki, na ripoti zako za mirabaha.
Unachohitaji ili kufuzu
Takriban wasikilizaji 15,000 wa kila mwezi: kiwango cha kuanzia, lakini si sharti kali.
Unamiliki masters zako (rekodi asili za nyimbo zako) na una haki ya kuziuza. Kolabo si tatizo, ilimradi unajua mgawanyo wa mirabaha (splits).
Pokea ofa yako
Utapokea ofa kutoka kwetu inayoonyesha thamani ya kila wimbo.
Rekebisha ofa yako
Unachagua kuuza katalogi nzima au asilimia yake, na asilimia hiyo ni uamuzi wako. Hakuna kinachokufunga hadi useme ndiyo.
Tunashughulikia uhamisho huku wewe ukiendelea na muziki
Uhamisho wa kisheria, kuhamishia nyimbo kwa msambazaji wetu na kuitunza katalogi. Tunaendelea kuisimamia kwa muda mrefu, wakati wewe unaandaa kazi yako inayofuata.

Tunawekeza duniani kote, kwa haraka na kwa urahisi.

Uamuzi ni wako
Uza sehemu unayotaka
Uza katalogi nzima au sehemu yake, na asilimia unaiamua wewe. Baadhi ya wasanii huuza kila kitu. Wengine huuza sehemu na kubaki na iliyosalia.
Kwa takwimu zako
Tathmini kulingana na mapato halisi
Tunaangalia historia yako ya streaming: katalogi inaingiza kiasi gani na jinsi inavyoingiza. Haijalishi unatoka wapi au unamjua nani.
Hakuna makato
Malipo ndani ya siku chache baada ya kusaini
Siku chache, si miezi. Hakuna ada za maandalizi, hakuna gharama za usimamizi, hakuna kinachokatwa kwenye kiasi tulichokubaliana.
Baada ya mauzo
Tunaboresha katalogi tunazonunua
Pitching, playlists, sync, metadata: nyimbo zako zinatunzwa vizuri na unafahamika zaidi kama msanii.
Wasanii tunaofanya nao kazi

Tumewekeza kwenye mamia ya wasanii duniani kote

Baadhi ya wasanii walio kwenye katalogi ya Sonomo:

Picha na majina ya wasanii kutoka Spotify

Hakuna cha kurejesha. Hakuna masharti ya kukubana.

Tofauti na advance, tunamiliki tu kile tulichonunua. Mapato mengine yote ya katalogi yako ni yako.

Mauzo ya katalogi
Hakuna riba wala cha kurejesha
Hakuna ada wala makato kwenye kiasi tulichokubaliana
Mirabaha ya utunzi wako inabaki kwako
Uhuru kamili kwa nyimbo utakazoachia baadaye
Advance ya kawaida
Inakatwa kwenye mirabaha ya katalogi yako yote, na katalogi nzima inabaki imefungwa
Ada na makato ya hapa na pale
Masharti yanayobana kile unachoweza kuachia baadaye
Mikataba inayohitaji mwanasheria kuieleza
Maswali

Maswali tunayoulizwa zaidi

Jua katalogi yako ina thamani gani.

Utapokea ofa ya wimbo kwa wimbo ambayo unaweza kuirekebisha mwenyewe.